1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Droni za Urusi zatishia bandari za mto Danube nchini Ukraine

17 Agosti 2023

Licha ya mashambulio yaliyofanywa na ndege zisizokuwa na rubani za Urusi kwenye bandari muhimu, meli ya kwanza ya mizigo ya Ukraine iliweza kuondoka kupitia njia ya bahari nyeusi.

Ukraine Odessa | Containerschiff Joseph Schulte verlässt Hafen
Picha: Ukraine's Infrastructure Ministry Press Office/AP/picture alliance

Mashambulio ya droni yalilengamaghala ya nafakakwenye bandari muhimu ya mto Danube. Mashambulio hayo yaliyoharibu miundombinu yamelaaniwa na jumuiya ya kimataifa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hatua hiyo ni muhimu katika kurejesha uhuru wa usafirikwenye bahari nyeusi. Hivi karibuni Urusi ilijiondoa kwenye mkataba uliohakikisha usafirishaji wa ngano ya Ukraine.

Soma pia:Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameipongeza meli ya kwanza ya mizigo iliyoondoka Ukraine

Katika hotuba yake ya usiku wa kuamkia, Rais Zelenskyy amefichua kwamba serikali yake inaongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa ndege zisizo na rubani.