1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo washambulia maeneo muhimu ya kijeshi Sudan

14 Septemba 2025

Afisa mmoja wa jeshi la Sudan ameliambia shirika la habari la AFP kwamba droni kadhaa za wanamgambo wa RSF zimeshambulia vituo muhimu vya kijeshi na miundo mbinu ya raia nchini Sudan.

Sudan | Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan na Mohamed Hamdan Dagalo
Jenerali wa jeshi la taifa Sudan Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan akiwa na Mohamed Hamdan Dagalo kiongozi wa wanamgambo wa RSFPicha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Afisa huyo amesema mashambulizi hayo yalilenga makao makuu ya jeshi la Sudan pamoja na maghala ya mafuta Magharibi mwa Mto Nile.

Mashambulizi mengine pia yalilenga kambi ya jeshi la anga la Kenana na uwanja mdogo wa ndege Kusini Mashariki mwa mji wa Kosti. Kituo cha umeme cha Um Dubakir pia kilishambuliwa.

Tangu Aprili mwaka 2023, Sudan imekuwa ikipambana na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la taifa na wanamgambo wa kundi la RSF.

Vita hivyo hadi sasa vimesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku mamilioni ya wengine wakipoteza makaazi yao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW