Droo ya awamu ya mchujo ya Champions League
16 Desemba 2013Droo ya awamu ya timu 16 bora ya UEFA Champions League, imefanywa leo katika makao makuu ya shirikisho la Soka Ulaya, mjini Nyon Uswisi. Mabingwa mara tisa wa Ulaya Real Madrid watashuka dimbani na timu ya Bundesliga Schalke 04, wakati makamu bingwa wa msimu uliopita Borussia Dortmund wakikutana na Zenit St Petersburg wa Urusi.
Mabingwa mara tatu Manchester United wa Uingereza watakabana koo na mabingwa wa Ugiriki Olympiakos, huku mabingwa mara saba AC Milan wa Italia wakicheza na Atletico Madrid wa Uhispania. Bayer Leverkusen wa Ujerumani wakutana na miamba wa Ufaransa Paris St Germain, nao Cheslea wa Uingereza wakimkaribisha tena Didier Drogba na kikosi chake cha Galatasaray.
Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Februari 18 na 19, na 25 na 26. mikondo ya pili itakuwa Machi 11 na 12, na 18 na 19. fainali itakuwa mjini Lisbon mnamo Mei 24, katika uwanja wa Estadio da Luz
Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman