1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamilioni wakabiliwa kwa njaa kufuatia ukame nchini Kenya

10 Februari 2026

Katika wiki za hivi karibuni, picha za mifugo iliyokonda katika eneo kame karibu na mpaka wake na Somalia zimewashtua wengi katika eneo hilo ambalo linaathiriwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Kenya I ukame
Mfugaji akimnywesha maji ngamia nchini KenyaPicha: Luis Tato/AFP

Hali ya ukame imewaacha zaidi ya watu milioni 2 wakikabiliwa na njaa katika sehemu za Kenya, huku jamii za wafugaji ng'ombe kaskazini mashariki mwa nchi hiyo zikiwa zimeathiriwa zaidi, hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Katika wiki za hivi karibuni, picha za mifugo iliyokonda katika eneo kame karibu na mpaka wake na Somalia zimewashtua wengi katika eneo hilo ambalo linaathiriwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Athari hizo zinatajwa kuenea hadi katika nchi za Somalia, Tanzania na hata Uganda, ambapo wengi wako hatarini kutokana na hali mbaya ya hewa na uhaba wa maji, Shirika la Afya Duniani lilisema mwishoni mwa Januari.

Wataalamu wanasema mengi yanayotokea yanatokana na mabadiliko ya tabianchiyanayoendelea kushuhudiwa duniani.
 
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW