1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dunia bado imegawika kuhusu ufadhili katika mkutano wa COP29

21 Novemba 2024

Rasimu mpya ya mkataba wa Tabianchi iliyotangazwa kwenye mkutano wa COP29 nchini Azerbaijan imeshindwa kutatua mkwamo kuhusu ufadhili.

COP29
Mkutano wa COP29Picha: Sean Gallup/Getty Images

Rasimu mpya ya mkataba wa Tabianchi iliyotangazwa kwenye mkutano wa COP29 nchini Azerbaijan imeshindwa kutatua mkwamo kuhusu ufadhili, huku mataifa yakigawanyika kuhusu makubaliano ya ufadhili wa dola trilioni moja, yanayotarajiwa kuchukua nafasi ya ahadi ya kila mwaka ya dola bilioni 100 iliyotolewa na mataifa tajiri kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Rasimu hiyo mpya haijaweka kiwango maalum cha fedha, hatua inayomulika migawanyiko ambapo nchi zinazoendelea zinataka dola trilioni 1.3 kila mwaka, hasa kutoka kwenye bajeti za serikali, huku mataifa tajiri yakishinikiza sekta binafsi kushiriki kikamilifu.

Soma: Mkutano wa COP29 waingia kipindi kigumu cha majadiliano

Masuala muhimu kama vyanzo vya fedha, njia za kukusanya, na ugawaji bado hayajatatuliwa, pamoja na hofu kwamba ahadi ya kupunguza matumizi ya mafuta ya visukuku iliyotolewa kwenye COP28 inapuuzwa. Huku mazungumzo yakikaribia mwisho, maafisa kutoka Umoja wa Ulaya, Marekani, na wadau wengine wakuu wanaendelea kuchukuwa tahadhari, huku wanaharakati wakikosoa ukosefu wa ahadi thabiti kama kushindwa kukabiliana na mahitaji ya haraka ya tabianchi.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW