1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dunia si mahala salama kwa wakimbizi - AI

24 Mei 2013

Ripoti ya Amnesty International ya mwaka huu juu ya hali ya wakimbizi na wahamiaji duniani inasema dunia imekuwa sehemu ya hatari kwa watu hao kwa sababu serikali za mataifa zimeshindwa kulinda haki zao

Flüchtlinge aus Mali im Flüchtlingslager in Maingaize im Niger an der Grenze zu Mali, aufgenommen am 20.04.2012. In Scharen laufen die Malier vor Putschisten und Rebellen davon. Viele sind nach Niger geflohen - dabei kämpft das Land selbst mit einer verheerenden Dürre. Im Flüchtlingslager erzählen sie von den schrecklichen Dingen, die sie erlebt haben. (Zu dpa "Flucht vor der Scharia: Malier suchen Schutz in der Dürre von Niger"). Foto: Carola Frentzen
Dürre im NigerPicha: picture-alliance/dpa

Akizungumza na shirika la habari la AFP, Katibu Mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty's International, Salil Shetty, amezitupia lawama serikali kwa kutothamini na kulinda haki za wakimbizi pamoja na wahamiaji katika nchi ambazo wanakimbilia au kuhamia, na badala yake nchi hizo zinatilia maanani maslahi yao.

"Kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kutafuta suluhu na kuzuia hali ya machafuko na migogoro inayo tokea sehemu tofauti dunia, kumesababisha hali ya kuwepo tabaka la watu wa hali ya chini na wengi wao wakimemo wakimbizi na wahamiaji, jambo ambalo linafanya wakimbizi na wahamiaji kuishi katika mazingira duni na yasiyo ya kiutu," alisema Shetty.

Akitoa mfano wa nchi ambayo hali ya wakimbizi na waahamiaji imekuwa mbaya Shetty alieleza "wakati dunia ina simama na kuangalia mapigano yanayo endelea nchini Syria, kati ya wapinzani wa serikali na jeshi la serikali, watu zaidi ya 80,000 wamesha poteza maisha na watu wengine million 4 kukimbia makaazi yao, na kati ya hao, million 1 na nusu wamekimbilia nje ya Syria nakuomba ukimbizi sehemu tofauti katika nchi za jirani, ambapo haki zao za kimsingi zimekuwa zikikiukwa."

Ulaya yalaumiwa

Vilevile katika ripoti hiyo, serikali za Ulaya zimelaumiwa kwa kutoangalia haki za wakimbizi na wageni, kufuatia hali ya ngumu za kiuchumi katika nchi hizo za Ulaya, jambo ambalo limefanya kuwepo na upungufu wa kazi na hivyo wahamiaji na wakimbizi kuonekana kama ndiyo chanzo cha tatizo la upungufu na ukosekanaji wa kazi.

Wakimbizi nchini Bangladesh.Picha: STRDEL/AFP/Getty Images

Akiongezea Katibu huyo wa Amnesty amesema "Hali ya kutoheshimiwa kwa haki za watu ambao wanaomba ukimbizi katika nchi za jumuiya ya Ulaya imeongezeka, na kutowa mfano wa kisa kilichoshuhudiwa nchini Italia mwaka 2012, ambapo mashua iliyokuwa imewabeba wakimbizi ilirudishwa ilikotoka, kwa madai ya kuwa mpaka waliopitia ulikuwa ni mpaka mtakatifu."

Shetty amesema wakimbizi na wahamiaji waliopo katika nchi za Jordan, Kuwait, Hong Kong na Lebanon "wamekuwa wakinyanyaswa, kijinsia, kiakili, wakati mwingine kubakwa na hata kunyimwa mishahara yao, kwani sheria zilizopo katika nchi hizo hazilindi maslahi ya wahamiaji na wakimbizi hao."

Katika ripoti hiyo, serikali za nchi zilizopo Kaskazini mwa bara la Afrika zimelaumiwa, na Misri ikitajwa kama mfano kwa kitendo ambacho kilifanywa na maafisa usalama wa nchi hiyo mwaka 2012, kwa kuwauwa watu wanane kwa kuwapiga risasi wakati walipokuwa wanajaribu kuvuka mpaka wa Sinai ili kuingia nchini Israel na watu wengi kukamatwa na kuwekwa kizuizini katika magereza ambayo hali zake za kifya ni mbaya.

Somalia tena

Somalia nchi ambayo imekuwa katika vita kwa muda wa miongo miwili, haikusahaulika katika ripoti ya Amnesty International, na kutajwa kuwa zaidi ya Wasomali millioni moja walilazimishwa kuyakimbia makaazi yao, na laki nne na nusu kati ya Wasomalia hao wanaishi katika moja ya kambi kumbwa ya wakimbizi duniani iliyopo katika mji wa Dadaab, kaskazini Mashariki ya nchi ya Kenya.

Wakimbizi wa Kisomali.Picha: AFP/Getty Images

Ripoti ya Amnesty's imesema "wakimbizi waliopo katika kambi ya Dadaab wamekuwa wakinyanyaswa, na kumekuwa na matukio mengi ya kubakwa kwa wanawake na wasichana wagodo."

Nchi nyingine ambazo zimetajwa kuvunja haki za wakimbizi na wahamiaji ni Gabon, Sudan, na Bahamas. Nchi Hizo zimeshutumiwa kwa kuwalazimisha wakimbizi kurudi makwao au wakati mwingine kuwaweka kizuizini na kuwasafirisha kwa kutumia nguvu.

Ikimalizia ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty's International limesema hadi kufikia sasa kuna wakimbizi wapatao million 15 na zaidi ya wahamiaji millioni mia mbili duniani kote.

Mwandishi: Rukundo Laurance/ AFPE/ APAE
Mhariri: Saumu Yusuf