Dunia yapata miezi 12 ya kwanza ya joto kuvuuka nyuzi 1.5C.
9 Februari 2024Matangazo
Dhoruba, ukame na matukio ya moto vimeikumba sayari ya dunia huku mabadiliko ya tabianchi, yakichangiwa na hali ya El Nino, yakisababisha joto kali katika mwaka wa 2023, na kuufanya kuwa wenye joto kali zaidi katika karibu miaka 100,000.
Hali hiyo imeendelea kushuhudiwa katika mwaka huu wa 2024, na shirika hilo la Ulaya linaloitwa Copernicus limethibitisha kuwa Februari 2023 hadi Januari 2024 kulishuhudiwa kupanda kwa joto hadi nyuzi 1.52 ikiwa zaidi ya hali ilivyokuwa kabla ya mapinduzi ya viwanda duniani.
Hata hivyo, shirika hilo limesema hiyo haimaanishi kwamba uvukaji huu wa kiwango cha joto duniani ni wa kudumu, na unaweza kushuka endapo hatua zitachukuliwa haraka.