1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Durov akubali Telegram kushirikiana na vyombo vya usalama

24 Septemba 2024

Mwanzilishi wa mtandao wa mawasiliano wa Telegram, Pavel Durov, amesema kuanzia sasa mtandao huo utakuwa unashirikiana na vyombo vya usalama kuwapa taarifa kuhusiana na uhalifu wa watumiaji wake.

Telegram Pavel Durov
Mwanzilishi wa Telegram, Pavel Durov.Picha: Albert Gea/File Photo/REUTERS

Durov, ambaye alikamatwa nchini Ufaransa mwezi uliopita kwa tuhuma za kushindwa kuchukuwa hatua dhidi ya wahalifu kwenye mtandao wake, alisema huduma ya kutafuta taarifa ya Telegram imetumika vibaya na watu wanaouza bidhaa haramu.

Kuanzia sasa, Telegram itakuwa inawapa maafisa wa usalama taarifa kama vile nambari ya simu na anwani ya mtandaoni ya wale wanaovunja kanuni za matumizi.

Soma zaidi: Mmilki wa Telegram ashtakiwa, mtandao wake si salama

Durov, mwenye umri wa miaka 39, yuko nje kwa dhamana, lakini haruhusiwi kutoka nje ya Ufaransa.

Kukamatwa kwake kulihusishwa na kukataa kwa mtandao wake kushirikiana na vyombo vya usalama juu ya masuala ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, biashara haramu ya binaadamu na udanganyifu wa mtandaoni.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW