1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru ya pili ya uchaguzi nchini Ufaransa , mgawanyiko wa mawazo.

Sekione Kitojo29 Aprili 2007

Duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Ufaransa inakaribia. Uchaguzi utafanyika hapo Mei 6. Lakini uchaguzi huo wa duru ya pili unapambanisha ncha mbili za mawazo , jinsi ya kupunguza idadi kubwa ya watu wasio na kazi , na kuwapa wapiga kura nafasi kubwa ya uhuru pamoja na usalama zaidi.

Wagombea wawili wa urais katika duru ya pili nchini Ufaransa kushoto Bibi Royal na Bwana Sarkozy.
Wagombea wawili wa urais katika duru ya pili nchini Ufaransa kushoto Bibi Royal na Bwana Sarkozy.Picha: AP Graphics

Mhafidhina Nicolas Sarkozy amewaambia wapiga kura , ambao wanaangalia suala la soko la nafasi za kazi kuwa katika nafasi ya juu katika mawazo yao, kuwa anaweza kutoa nafasi nyingi za kazi katika muda wa miaka mitano kutokana na hatua kali ambazo zitawafanya watu wapende kufanyakazi na waajiri waweze kuajiri zaidi.

Mgombea mwenzake msoshalist , Segolene Royal , pia ana nia ya kupambana na hali inayozidi kuongezeka ya kutokuwa na usalama katika kazi inayosababishwa na utandawazi na anapendekeza hatua ambazo zinakwenda mbali kupindukia upeo wa kujihami unaotolewa kwa wafanyakazi na kuyapa matumaini makampuni kuwaajiri wanafunzi waliomaliza shule ambao hawana ujuzi.

Wakosoaji wa hatua za Sarkozy wanasema kuwa mipango yake itaathiri wanyonge katika jamii, lakini mapendekezo yake yako karibu na mageuzi ambayo makundi ya ushauri ya kimataifa pamoja na wachumi wanasema yataangalia kwa kina matatizo ya mfumo wa soko la ajira nchini humo.

Kwa upande wa kiuchumi, unyumbulifu ni muhimu kuliko usalama kwa hivi sasa kutokana na hali inayojikuta Ufaransa , amesema Erik Nielsen , mchumi katika chuo cha Goldman Sachs mjini London.

Kwa lengo la ukuaji wa muda mrefu , mtu anahitaji kulifanya soko la ajira la pekee zaidi ili kuwa na soko kuwa kubwa na lenye kufanya kazi na Sarkozy hajagusa sehemu kubwa zaidi. Lakini unyumbulifu ni kitu muhimu kinachokosekana katika soko la ajira la Ufaransa, ameongeza.

Mkanganyiko mkubwa hivi sasa unakabili kiwango cha wasio na kazi nchini Ufaransa lakini wengi wanakubali kuwa ukosefu wa kazi unafikia kati ya asilimia 8.3 na 8.8. Hata kama utafanya makosa kwa upande wa chini , hii ni idadi ya juu ya nane katika bara la Ulaya.

Kwa upande fulani wa kulaumiwa ni sheria za kujihami za uajiri za nchi hiyo.Hali hii inaviza uwezo wa ujenzi wa nafasi za kazi, katika wakati ambapo nchi hiyo ambayo ni ya pili kwa kwa uchumi imara katika eneo linalotumia sarafu ya Euro inajiweka wazi kama mataifa mengineyo kwa mageuzi na upungufu wa nafasi za kazi hali inayoletwa na ongezeko la kupotea kwa mitaji, bidhaa na huduma.

Nchi nyingi za Ulaya ambazo uchumi wao umeimarika zinaweka msisitizo katika kuwalinda wafanyakazi, na kuwasaidia kupata kazi mbadala iwapo watapoteza kazi zao, na kuweka misingi ya mazingira bora ambayo inahakikisha kuwa nafasi mpya za kazi zinapatikana.

Mpango wa Sarkozy unashambulia tatizo hilo moja kwa moja na sio kama ugawaji upya wa mali, amesema Francois-Xavier Chevallier, mkuu wa mikakati katika shirika la hisa la CM-CIC.

Royal anataka kupanua mfumo wa saa 35 kwa wiki za kazi hadi katika makampuni madogo, na kuweka viwango kamili kwa ajili ya malipo ya ziada, kupandisha kiwango cha chini cha mshahara hadi Euro 1,500 katika muda wa miaka mitano, na kuondosha mikataba ya kazi ya CNE ambayo inaruhusu makampuni madogo kuajiri wafanyakazi kirahisi.