1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru zadokeza Zelensky kuitembelea Italia mwishoni mwa juma

12 Mei 2023

Vyombo vya habari vya Italia vimeripoti kwamba rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine anatafakari uwezekano wa kufanya ziara mjini Roma mwishoni mwa wiki hii

Ukraine Präsident Selenskyj PK
Picha: Sergei Supinsky/AFP

Kwa mujibu wa shirika la habari la Italia, ANSA,  iwapo Zelensky atafanya ziara hiyo, anapanga kukutana na waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni na kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis.

Soma zaidi:Papa Francis ataka vita vya Ukraine vikomeshwe haraka

Likinukuu duru za serikali ya Italia na kutoka makao makuu ya kanisa katoliki mjini Vatican, shirika hilo la habari limesema ziara ya Zelensky bado inajadiliwa ingawa hadi sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa. Kumekuwa pia na ripoti kwamba kiongozi huyo wa Ukraine ataitembelea Ujerumani mwishoni mwa juma hili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW