DW Kiswahili yamuomboleza Mohammed Abdulrahman
16 Julai 2025
Matangazo
Mohammed aliaga dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Cologne, Ujerumani. Kabla ya kustaafu mwaka 2019, Mohamed alikuwa Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili na mhariri maarufu aliyetoa mchango mkubwa kwa kizazi cha wanahabari.
Waliomfahamu wanamkumbuka kama mwandishi mahiri, mlezi, na mjenzi wa Kiswahili fasaha na sanifu ndani ya DW. Alijulikana si tu kwa sauti yake hewani, bali kwa umahiri wake wa kuandika na kufundisha. Mohammed Abdulrahman ameacha alama isiyofutika.