1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DW yatangaza kubana matumizi kufuatia punguzo la bajeti

19 Februari 2026

Shirika la kimataifa la utangazazi la Ujerumani DW limetangaza kuwa linalazimika kuokoa kiasi cha Euro milioni 21 baada ya kupunguziwa bajeti na serikali ya shirikisho.

Ujerumani Bonn 2025 | Makao makuu ya DW
Makao makuu ya DW BonnPicha: Michael Nguyen/NurPhoto/picture alliance

Shirika la kimataifa la utangazazi la Ujerumani DW limetangaza kuwa linalazimika kuokoa kiasi cha Euro milioni 21 baada ya kupunguziwa bajeti na serikali ya shirikisho.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano, DW imesema kwamba "takribani nafasi 160 za kudumu zitaathirika", lakini ikaongeza kwamba hakutokuwa na ufutaji kazi.

Hatua hizi zinakuja mnamo wakati ruzuku inayotolewa na serikali ya shirikisho kwa DW kupunguzwa kwa euro milioni 10 hadi kufikia euro milioni 415 mwaka 2026, kwa mujibu wa DW, ambayo hufadhiliwa na serikali ya Ujerumani lakini hufanya kazi bila kutegemea serikali.

Mkurugenzi wa DW Barbara Massing akizungumza mjini BerlinPicha: Boris Geilert/DW

DW pia inakabiliwa na gharama za nyongeza takribani euro milioni 11 kutokana na kupanda kwa mishahara. "Kwa sababu hiyo, DW inahitajika kupunguza matumizi kwa jumla ya €21 milioni. Akiba hiyo itatekelezwa kwa njia bora ya kijamii na kwa mujibu wa vipaumbele vya kimkakati vya DW. Maeneo mengi ya shirika yataathirika."

Tofauti na mashirika ya umma ya utangazaji ya ARD na ZDF, DW haifadhiliwi na ada ya leseni za watumiaji, bali moja kwa moja na mapato ya kodi.

Vipindi vyake vinatangazwa katika lugha zaidi ya 30 na vinalenga kuchora taswira halisi ya Ujerumani, kukuza mazungumzo ya kimataifa na kuimarisha maadili ya kidemokrasia.

Chini ya mpango wa kubana matumizi, DW imeamua kusimamisha Idhaa yake ya Kigiriki huku idara nyingine za uandishi wa habari katika lugha zingine zikitarajiwa kuathirika ikiwemo Idhaa za Kireno kwa Afrika na Dari/Pashto kwa Afghanistan.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW