1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dzeko aweka rekodi na klabu ya Schalke

26 Januari 2026

Edin Džeko ndiye mfungaji mkongwe zaidi katika historia ya Bundesliga daraja la pili kwa bao lililoisadia Schalke kurudi mchezoni dakika za mwisho dhidi ya Kaiserslautern akiwa na umri wa miaka 39 na siku 314.

Edin Džeko amekuwa mfungaji mkongwe zaidi katika historia ya Bundesliga daraja la pili akiwa na umri wa miaka 39 na siku 314.
Edin Džeko amekuwa mfungaji mkongwe zaidi katika historia ya Bundesliga daraja la pili akiwa na umri wa miaka 39 na siku 314.Picha: Rolf Vennenbernd/dpa/picture alliance

Edin Dzeko alifunga bao katika mechi yake ya kwanza na klabu yake ya Schalke na kuwasaidia vinara wa ligi ya daraja la pili ya Ujerumani kupambana na kutoka sare ya 2-2 nyumbani Veltins Arena mjini  Gelsenkirchen dhidi ya Kaiserslautern siku ya Jumapili.

Mshambuliaji huyo wa Bosnia aliyesafiri sana, ambaye aliwahi kushinda taji la Bundesliga na klabu ya Wolfsburg katika kipindi chake cha awali nchini Ujerumani mwaka wa 2009, alifunga bao dakika ya 87 baada ya kutoka benchi na kupunguza pengo.

Kenan Karaman alifunga bao dakika ya 90 baada ya bao la Ivan Prtajin kuwapa wageni uongozi wa 2-0.

Schalke inabaki kileleni kwa ligi ya daraja la pili ya Bundesliga kwa pointi mbili lakini bado haijashinda mwaka huu wa 2026 baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Hertha Berlin wikendi iliyopita.

Zaidi ya mashabiki 62,000 walimkaribisha kwa furaha Dzeko dakika ya 67 na mchezaji huyo wa miaka 39 alileta mabadiliko haraka.

"Inaonekana kama ushindi," Dzeko aliambia Sky. "Timu ilionyesha tabia nzuri sana."

Usajili wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City na Roma kutoka Fiorentina unaonekana kama mapinduzi kwa Schalke huku wakitarajia kurudi katika ligi kuu ya Bundesliga baada ya misimu mitatu nje ya ligi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW