1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EAC yaiomba DRC kufanya mazungumzo ili kumaliza mzozo

30 Januari 2025

Jumuiya ya Afrika Mashariki imeitolea mwito Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kufanya mazungumzo na pande zote zinazohusika na mzozo wa mashariki mwa nchi hiyo wakiwemo M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.

Tanzania Arusha Mkutano wa EAC
Baadhi ya wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye mkutano wa kilele mjini ArushaPicha: Philbert Rweyemamu/EAC

Rai hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao usiku wa kuamkia leo, ambao hata hivyo ulisusiwa na Rais Felix Tshisekedi wa Kongo.

Kiongozi huyo badala yake alitoa hotuba kwa taifa akisema vikosi vya nchi hiyo vinaendelea kupambana na waasi wa M23 wanaosonga mbele mashariki mwa nchi hiyo na kuilaumu jumuiya ya kimataifa kwa kutochukua hatua.

Mapigano ya wiki kadhaa yaliyoshuhudia waasi wa M23 wakikamamata maeneo makubwa ndani ya Kongo, yamezusha miito ya kufanyika mazungumzo ya amani ili kuepusha janga la kibinadamu linanaloweza kutokea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW