ECOWAS wasitisha mkutano muhimu wa kijeshi juu ya Niger
12 Agosti 2023Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, walikuwa wakutane leo katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi kwenye jumuiya hiyo. Lakini jioni ya jana, kulitolewa tamko la kuuakhirisha mkutano huo kwa muda usiojulikana.
Soma zaidi: ECOWAS waamua kujizuia kuingilia kati kijeshi Niger
Vyanzo hivyo vinasema mkutano huo ulikuwa umeandaliwa ili kuwaeleza viongozi wa ECOWAS juu ya "njia bora zaidi" za kuunda na kutuma kikosi hicho cha dharura nchini Niger. Bado ECOWAS haijafafanuwa undani wa kikosi hicho wala ratiba ya hatua zake, huku viongozi wake wakisisitiza kuwa bado wanataka suluhisho la amani. Ahirisho la mkutano huo lilitangazwa wakati maelfu ya wananchi wa Niger wakikusanyika kuunga mkono jeshi lao mbele ya kituo kimoja cha jeshi la Ufaransa jana Ijumaa. Mkoloni huyo wa zamani ana wanajeshi zaidi ya 1,500 nchini humo.