ECOWAS wautambua utawala wa kijeshi wa Niger
11 Desemba 2023Matangazo
Katika mkutano wa kilele uliofanyika siku ya Jumapili (Disemba 10) mjini Abuja, Nigeria, viongozi hao wa ECOWAS waliutambua rasmi utawala huo wa kijeshi, ingawa walitaka kipindi hicho cha mpito kiwe kifupi, ili waweze kuulegezea vikwazo vya kiuchumi walivyouwekea.
Soma zaidi: Viongozi wa ECOWAS wakutana kujadili muelekeo wa mataifa yaliyo chini ya utawala wa kijeshi
Rais wa Kamisheni ya ECOWAS, Omar Touray, aliwaambia waandishi wa habari kwamba viongozi wa mataifa ya Benin, Togo na Sierra Leone, wamekabidhiwa jukumu la kuendeleza mazungumzo na baraza la kijeshi la Niger yatakayoamuwa juu ya uondolewaji wa vikwazo.
Utawala wa kijeshi wa Niger umekuwa ukisema kwamba unahitaji angalau miaka mitatu kuirejesha nchi kwenye utawala wa kiraia.