1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ecuador watambwaga Messi Copa America robo fainali?

1 Julai 2024

Huko Amerika mashindano ya kuwania ubingwa wa bara hilo Copa America yanaendelea na Ecuador wametinga hatua ya robo fainali.

Copa America Fußball Argentinien Kanada Moïse Bombito
Nahodha wa Argentina Lionel MessiPicha: Jason Allen/AP Photo/picture alliance

Hii ni baada ya kutoka sare ya kutofungana na Mexico katika mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia Jumatatu.

Ecuador ambao wanatafuta kufuzu nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu walipokuwa wenyeji wa mashindano hayo mwaka 1993, watakuwa na kibarua katika hatua hiyo ya nane bora kwani watakuwa wanapambana na mabingwa watetezi Argentina ambao wanaongozwa na Lionel Messi.

Mabingwa wa kundi lao Venezuela waliowarambisha Jamaica magoli 3-0 watakuwa wanachuana na Canada katika mechi ya robo fainali.

Jumanne usiku kutakuwa na mechi mbili ambapo Bolivia watacheza na Panama katika mechi ya kwanza kisha mtanange wa pili uwapatanishe Marekani na Uruguay.

Vyanzo: Reuters/DPAE