1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUlaya

Uchafuzi wa hewa wasababisha vifo zaidi ya laki mbili Ulaya

24 Novemba 2023

Chembechembe zitokanazo na uchafuzi wa hewa zimesababisha vifo vya karibu watu 250,000 kote barani Ulaya mnamo mwaka 2021.

Mwanaume akiwa kavalia barakoa kujikinga na hewa chafu
Mwanaume akiwa kavalia barakoa kujikinga na hewa chafuPicha: Morteza Nikoubazl/NurPhoto/picture alliance

Hayo ni kulingana na ripoti iliyotolewa hii leo na Shirika la mazingira la Umoja wa Ulaya EEA.

Shirika la EEA limewasilisha matokeo hayo katika kongamano la nne la kuhimiza Hewa Safi lililofanyika mjini Rotterdam, Uholanzi na kusema vifo hivyo vingeliweza kuepukika ikiwa mataifa ya Ulaya yangeliheshimu viwango vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Soma pia

Mkurugenzi mtendaji wa EEA Leena Ylä-Mononen amesema ingawa Ulaya imepiga hatua kubwa katika miaka iliyopita ili kupunguza viwango vya uchafuzi wa hewa, takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa athari ya uchafuzi huo kwa afya bado ni kubwa mno.

Kulingana na makadirio ya EEA, chembechembe hizo husababisha magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari, pumu na saratani ya mapafu.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW