Ehud Barak atikisa siasa za Israel
24 Agosti 2015Katika mahojiano yaliofichuliwa ambapo Barak pia anamtaja waziri mkuu Benjamin Netanyahu kama asiyeweza kufanya maamuzi na asiye na mtu asiyeweza kuleta matumaini yalikuwa gumzo la kubwasiku ya Jumapili nchini Israel na kuashiria huenda Barak ana nia ya kurudi tena madarakani siku zijazo.
Akiwa pia waziri mkuu wa zamani, Barak anatajwa kama kiongozi wa mwisho wa mrengo wa kadri wa chama cha Labour kushinda uchaguzi,alipomshinda Netanyahu mwaka 1999.Lakini anaonekana na wachambuzi kama aliyepoteza kipindi chake kilichodu miaka miwili tu , kilichoibua hisia za kuwa mtu mwerevu lakini jeuri, taabu kumchambua na aliyekuwa na mizengwe isiyo na kikomo.
Lakini Barak baadaye alirejea siasani, akahudumu kama waziri wa ulinzi kutoka mwaka 2007 hadi 2013,wakati alipoungana na Netanyahu aliyechaguliwa tena na kupinga mipango ya Nyuklia ya Iran. Aliondoka kwenye siasa kwani chama cha Labour kilikuwa dhaifu na kilichogawika.Sasa akiwa na miaka 73 huenda Barak asiwe na fursa nyingine ya kurejea kwenye uongozi.
Afichua siri za serikali
Mahojiano na Barak,yaliovuja mnamo siku ya Ijumaa kupitia Televisheni ya Channel 2 yanashabihiana na kujiri kwa wasifu wake ambao umefanya aangaziwe tena. Mchambuzi mkongwe Rina Mazliach alikiambia kituo hicho cha kibinafsi kuwa anashangaa kuwa Barak anataka kurejea katika siasa.Katika mahojiano hayo yaliyofichuka Baraka aliangazia moja wapo wa siri za nchi-ikiwa Israel ilikuwa tayari kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya mradi wa nyuklia wa Iran.
Kwa miaka mingi yeye na Netanyahu walitoa vitisho kushambulia iwapo ulimwengu hautachukuwa hatua.Vitisho hivyo vilipuuzwa na wachambuzi kuwa ni kelele tu lakini vikaonekana ndivyo vilishawishi ulimwengu kuiwekea Iran vikwazo.
Kwenye mahaojiano hayo Barak alisema kuwa yeye na Netanyahu walipendelea mashambulizi mwaka 2010 lakini mkuu wa majeshi Gabi Ashkenazi alisema Israel haikuwa na uwezo kufanya mashambulizi hayo.Barak alisema haungetaka kujuta kutokana na ushauri wa mkuu wa majeshi.
Miaka kadhaa baadae ,Barak alisema mawaziri wawili wenye ushawishi walikuwa na wazo lingine na kulizima shambulizi. Halafu 2012 pamoja Kulifanyika luteka ya kijeshi ya pamoja na vikosi vya Marekani na ziara na ikapangwa ziara ya waziri wa ulinzi wa Marekani wakati huo Leon Panetta .
Kulingana na kituo cha televisheni cha Channel 2 Barak alijaribu kuzuia kituo hicho kupeperusha mahojiano hayo,lakini ofisi ya kijeshi ikawapa idhini.Hakukuwa na taarifa yoyote siku ya Jumapili kutoka kwa Barak,Netanyahu au Ashkenazi ambaye alikuwa mkuu wa majeshi. Mawaziri waliokuwa wametajwa na Barak ambao ni Yuval Steinitz na waziri wa ulinzi Moshe Yaalon pia walikataa kutoa maoni yoyote.
Lakini Avigdor Lieberman aliyekuwa waziri wa maswala ya nchi za kigeni wa Israel,alionekana kumuunga mkono Barak kwenye mahajiano yake na kituo hicho. "Ikiwa waziri mkuu hawezi kupitisha jambo kwenye baraza lake la mwaziri basi kuna tatizo".Lieberman alisema siku ya Jumapili.
Ataka kusafisha jina
Danny Dor mmoja wa waandishi wa kitabu kipya alisema Baraka alijua anarekodiwa na hakukuwa na ahadi kuwa mambo hayo hayangechapishwa. Baadhi wamehoji kuwa Barak alijua alichokuwa anafanya kwenye mahojiano hayo. Lakini kilicho wazi ni kwamba kuna nia fulani kulingana na mchambuzi mmoja wa gazeti la Yediot Ahronot.
Barak huenda anataka kubadili kuimarisha sifa yake iliyoharibika na kurejea katika historia.Lakini matamshi haya yanajiri huku Israel ikitafuta kiongozi ambaye atampa Netanyahu ushindani hasa kwa ajili ya Wapalestina na pia nchi hiyo inaposogelea njia ya kutopenda mabadiliko na pia dini.
Mtu anayepigiwa upatu kushika nafasi ya Isaac Herzog kama kiongozi wa Labour baada ya Herzog kushindwa uchaguzi uliopita na Netanyahu mwezi Machi, ni Ashkenazi , mkuu wa wa zamani wa majeshi ambaye ametajwa na Baraka kwenye mahojiano kuwa alipinga mashambulizi dhidi ya Iran.
Mwandishi: Bernard Maranga /APE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman