Ehud Olmert akutana na viongozi wa Palestina,Jordan na Misri
25 Juni 2007Viongozi hao wanakutana kwenye kitongoji cha burdani cha Sharm el Sheikh takriban wiki mbili baada ya Hamas kutwaa madaraka katika Ukanda wa Gaza na rais wa mamlaka ya Palestina bwana Mahmoud Abbas kutangaza serikali mpya ya dharura.
Hatahivyo waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema kuwa watu wasiweke matumaini makubwa juu ya mkutuno huo .Lakini wadadisi wanasema mkutano huo utaimarisha msimamo wa rais Mahmoud Abbas katika mvutano wake na chama cha Hamas.
Kila hatua inachukuliwa kwa shinikizo la Marekani ili kumuimarisha rais Abbas Baraza la mawaziri la Israel limeidhinisha hatua ya kuachilia fedha kiasi cha dola milioni 350 kwa ajili ya serikali mpya ya dharura ya Palestina.Fedha hizo zinatokana na kodi zilizozuiwa na Israel kwa lengo la kuidhoofisha serikali ya Hamas.
Wawakilishi wa Hamas hawakualikwa kuhudhuria mkutano huo wa Sharm el Sheikh.Msemaji wa chama hicho bwana Barhum ameeleza kuwa chama chake kinapinga mkutano huo .kwa sababu hauzingatii malengo ya wapalestina .
AM.