1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Ekrem Imamoglu, kuhojiwa dhidi ya madai ya ujasusi

26 Oktoba 2025

Meya wa Istanbul aliyefungwa Jela Ekrem Imamoglu, alipelekwa katika mahakama moja mjini humo kuhojiwa kama sehemu ya uchunguzi mpya ulioanzishwa kubaini madai dhidi yake ya ujasusi.

Ekrem Imamoglu
Meya wa Istanbul aliyefungwa Jela Ekrem ImamogluPicha: Yasin Akgul/AFP

Mamia ya wafuasi wake walikusanyika nje ya mahakama hiyo, kumuunga mkono kiongozi huyo wa upinzani ambaye ni mpinzani na mkosoaji mkubwa wa serikali ya rais Recep Tayyip Erdogan.

Uchunguzi huo dhidi ya madai ya ujasusi ulioanzishwa siku mbili zilizopita, unaoanishwa na kampeni ya kisiasa ya meya  Imamoglu na mwanamume mmoja aliyekamatwa mwezi Julai akidaiwa kufanya shughuli za kijasusi kwa niaba ya mataifa ya kigeni.

Meneja wake wa kampeni  Necati Ozkan na muandishi habari Merdan Yanardag  pia wanatarajiwa kuhojiwa kama sehemu ya uchunguzi huo mpya.

Imamoglu anashikiliwa tangu mwezi Machi kwa madai ya ufisadi, madai aliyoyakanusha vikali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW