EL-ASSAD AALIKWA TENA NA KATZAV:
14 Januari 2004Matangazo
JERUSALEM: Rais wa Israel Mosche Katzav kwa mara nyingine tena amemualika Rais Basher el-Assad wa Syria kwa majadiliano ya amani.Katzav akizungumza na Al Jazeera stesheni ya televisheni ya kiarabu,amesema mazungumzo hayo yanaweza kufanywa kwa siri au kutangazwa rasmi na bila ya kuwepo masharti.Siku ya jumatatu Katzav alikwisha mualika el-Assad kwa mazungumzo mjini Jerusalem,lakini serikali ya Damascus imekataa ikisema kuwa mualiko huo hauna uzito. Kwa upande mwingine waziri mmoja katika serikali ya Israel ameeleza wazi wazi kuwa Israel haina nia ya kuirejeshea Syria Milima ya Golan iliotekwa wakati wa vita vya mwaka 1967.Eneo hilo muhimu la mpakani ni kiini cha mzozo,kati ya Syria na Israel.
