1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipchoge bingwa tena

29 Aprili 2019

Eliud Kipchoge ameweka rekodi ya kushinda marathon ya London kwa mara ya nne Jumapili. Kipchoge alishinda kwa kuandikisha muda wa 2:02:37, huo ukiwa muda wa pili wa kasi kihistoria katika marathon.

Leichtathletik London Marathon | Eliud Kipchoge
Picha: picture-alliance/Actionplus/J. P. FletcherS

Kipchoge ndiye anayeshikilia rekodi ya kasi zaidi katika marathon baada ya kuandikisha muda wa kasi zaidi duniani alipokimbia kwa 2:01:39 katika marathon ya Berlin, Ujerumani mwaka jana.

Mkenya huyo amekimbia jumla ya marathon 12 na kushinda 11.

Eliud Kipchoge akiwa na mshindi wa kina dada Bridget Kosgei pamoja na mwanamfalme Harry Picha: picture-alliance/Newscom/J. Mochizuki

Muingereza Sir Mo Farah ambaye wengi walitazamia ampe ushindani mkubwa Kipchoge, hakufua dafu na akamaliza katika nafasi ya tano.

Upande wa wanawake bingwa mtetezi Vivian Cheruiyot kutoka Kenya aliishia kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Bridget Kosgei.