1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eliud Kipchoge ashinda tuzo ya Asturias

18 Mei 2023

Mwanariadha mashuhuri wa Kenya Eliud Kipchoge, ameshinda tuzo ya mwaka huu ya binti wa Mfalme wa Austurias ya Michezo.

Eliud Kipchoge gewinnt Berlin Marathon
Picha: Christoph Soeder/AP

Shirika la Uhispania linalosimamia tuzo hiyo, limetangaza hayo leo.

Kipchoge mwenye umri wa miaka 38 ambaye ameshinda medali za dhahabu katika mbio za masafa marefu za mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 na 2020, anachukuliwa kuwa mwanariadha bora ulimwenguni wa mbio za masafa marefu.

Aliwahi pia kushinda mbio za mita elfu 5,000 katika mashindano ya ulimwengu mwaka 2003.

Shirika hilo limesema Kipchoge ambaye pia ameshinda mashindano ya Berlin na London marathion mara nne, anafahamika kama mwanafalsafa kutokana na juhudi na mikakati yake kwenye mashindano.

Tuzo hiyo yenye thamani ya euro 50,000, ni kati ya tuzo nane ambazo hukabidhiwa waliofanya vyema katika Nyanja za Sanaa, mawasiliano, sayansi na fasihi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW