Macron aanza ziara ya siku tatu Uingereza
8 Julai 2025
Matangazo
Kando ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo, Starmer na Macron watazungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kuongeza bajeti ya ulinzi na juhudi za pamoja za kukabiliana na wahamiaji haramu.
Macron atakutana pia Mwanamfalme William na mkewe kabla ya kuelekea katika Kasri la Windsor kukutana na Mfalme Charles na mkewe Camilla.
Starmer na Macron wanatarajiwa kufanya mkutano na nchi washirika Alhamisi 10.07.2025 kujadili msaada zaidi kwa Ukraine na namna ya kuishinikiza zaidi Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine. Watazungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni.