1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Macron kukutana na Scholz na Andrzej Duda kuijadili Ukraine

12 Juni 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo atawapokea mjini Paris Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Poland Andrzej Duda ili kujadili msaada zaidi kwa Ukraine na kuandaa mkutano wa kilele wa NATO mwezi ujao

China France Präsident Emmanuel Macron
Picha: Ng Han Guan/AP Photo/picture alliance

Ukraine inatarajia katika mkutano huo zifikiwe hatua madhubuti kuhusu nia yake ya kujiunga na NATO huku mataifa kama Marekani na Ujerumani yakidhihirisha wasiwasi wao na wakati huo huo yakihofia  hatua isiyotabirika inayoweza kuchukuliwa na Urusi.

NATO yaanza mazoezi makubwa ya jeshi lake la anga nchini Ujerumani

NATO inaanza leo mazoezi makubwa ya jeshi lake la anga nchini Ujerumani, ili kudhihirisha umoja baina ya nchi wanachama na uwezo pia wa kukabiliana na vitisho hususan kutoka Urusi. Luteka hizo zitakazojumuisha ndege za kivita 250 kutoka mataifa 25 na washirika wengine, zitaendelea hadi Juni 23, na karibu watu 10,000 watashiriki.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW