1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eneo la kuhifadhi mafuta Crimea lashambuliwa

29 Aprili 2023

Gavana aliyeteuliwa na serikali ya Urusi katika Rasi ya Bahari Nyeusi, Mikhail Razvozhayev amesema moto mkubwa ulizuka kwenye eneo la kuhifadhia mafuta la Crimea baada ya kushambuliwa na ndege isiyo na rubani.

Krim l Hauptstadt Simferopol
Picha: Alexei Konovalov/TASS/dpa/picture alliance

Kupitia ukurasa wake wa telegram gavana huyo amechapisha vidio na picha za tukio hilo. Amesema kutokana na kiwango kikubwa cha moto shughuli ya kuuzima moto huo ni ngumu.Hata hivyo hakusema iwapo ndege hiyo inayorushwa bila ya rubani anayodai ilisababisha moto huo ni ya jeshi la Ukraine au la. Mwaka 2014 Urusi iliinyakua Crimea, hatua ambayo sehemu kubwa ya ulimwengu inaitazama kama kinyume cha sheria.Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekwisha sema kuwa taifa lake lipo katika jitihada ya kulirudisha eneo hilo katika himaya yake katika kipindi hiki cha uvamizi kamili wa Urusi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW