1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bwawa la Kakhovka lasababisha mafuriko makubwa

8 Juni 2023

Eneo lenye ukubwa wa kilomita 600 za mraba katika mkoa wa Kherson wa kusini mwa Ukraine limefurika maji, baada ya kuharibiwa kwa bwawa la umeme la Kakhovka.

Ukraine nach Zerstörung von Kachowka Staudamm
Picha: Andre Alves/picture alliance/AA

Gavana wa mkoa huo, Oleksandr Prokudin amesema asilimia 86 ya sehemu iliyoathiriwa iko chini ya udhibiti wa Urusi, kwenye ukingo wa kushoto wa mto Dnipro. Kina cha wastani cha maji ya mafuriko hayo kilikuwa cha mita 5.61  mkoani Kherson siku ya Alhamis. Mwanaharakati wa mazingira kutoka shirika la Greenpeace Denys Tsutsaiev amesema hali hiyo inatishia baioanuai.

Watu wahama eneo la mafuriko

Kupitia mkanda wa video, gavana wa Kherson Oleksandr Produkin amesema watu wapatao 2000 walikuwa wameondoka katika eneo la mafuriko hadi leo asubuhi, na kuongeza kuwa licha ya kitisho cha mashambulizi ya Urusi, shughuli za kuwahamisha watu zinaendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW