Eneo muhimu la visima vya mafuta kufunguliwa tena Libya
5 Machi 2019Matangazo
Moja kati ya maeneo muhimu ya visima vya mafuta nchini Libya yanatarajiwa kufunguliwa karibu miezi mitatu baada ya kutekwa na kundi lenye silaha.
Shirika linalomilikiwa na serikali la mafuta limesema katika taarifa jana kwamba utoaji mafuta katika eneo la Al-Sharara kusini mwa Libya unatarajiwa kuanza katika muda wa wiki chache zijazo.
Tangazo hilo linafikisha mwisho, hatua maalum ya kisheria iliyotangazwa mwezi Desemba ambayo ililiondolea shirika hilo jukumu la kushindwa kutimiza mikataba.
Kuanzisha utoaji wa mafuta tena kunafuatia kuondolewa kwa makundi yenye silaha yanayohusika na kuzuwia uzalishaji, shirika hilo limesema, hali iliyosababisha upotevu wa dola bilioni 1.8.