1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Euro 2024: Ni England au Uhispania leo?

Angela Mdungu
14 Julai 2024

Timu za taifa za Uhispania na England zitachuana baadaye leo katika mchezo wa fainali ya michuano ya kandanda ya EURO 2024 utakayofanyika mjini Berlin.

Mchezaji nyota wa Uhispania Lamine Yamal aliyetimiza miaka 17 wiki hii
Mchezaji nyota wa Uhispania Lamine Yamal aliyetimiza miaka 17 Jumamosi ya Julai 13,2024Picha: Bradley Collyer/empics/picture alliance

Mechi hiyo iliyopangwa kuchezwa saa nne usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki na saa tatu usiku kwa saa za Ulaya ya kati, inatarajiwa kuhudhuriwa na Mwanamfalme wa Uingereza William, Mfalme Felipe wa Uhispania, Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez na Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer.

Uhispania inawania kushinda ubingwa huo kwa mara ya nne ikiwa na mchezaji wake nyota Lamine Yamal aliyetimiza miaka 17 jana Jumamosi. Kwa upande wake England inayodai kuwa ndiko soka lilikozaliwa, haijawahi kushinda kombe lolote kubwa tangu walipojinyakulia kombe la dunia mnamo mwaka 1966.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW