1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

England wapata ushindi mwembamba dhidi ya Haiti

22 Julai 2023

Mabingwa wa kombe la Euro 2022 England wameanza kampeni yao ya kuwania Kombe la Dunia la wanawake kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Haiti ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza.

Frauen Fußball WM 2023 | England v Haiti
Picha: DAN PELED/REUTERS

Bao la ushindi lilitiwa kimyani na mchezaji Georgia Stanway kupitia mkwaju wa penalti kunako dakika ya 29 ya mchezo.

Katika mechi ya kundi E Marekani imeilaza Vietnam 3-0 katika uga wa Eden Park huku Denmark ikisajili ushindi wa bao 1-0 katika mechi za kundi D.

Soma pia:Zambia yagaragazwa 5-0 na Japan 

Sambamba na mabingwa watetezi Marekani, England ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kubeba kombe hilo, katika mashindano haya yalioandaliwa Australia na New Zealand.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW