1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

England yatinga nusu fainali Euro 2020

4 Julai 2021

Timu ya England imefuzu nusu fainali ya michuano ya kuwania kombe la Ulaya, EURO 2020 baada ya kuiadhibu Ukraine mabao 4-0.

EURO 2020 | Ukraine vs England | Tor Henderson
Picha: Alberto Lingria/REUTERS

Baada ya kuinyuka Ukraine mabao 4-0 katika robo fainali ya Euro 2020, hivyo kujikatia tiketi kuingia nusu fainali, England sasa itakutana na Denmark katika juhudi za kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali ya kwanza tangu waliposhinda kombe la dunia mwaka 1966.

Kocha wa Uingereza Gareth Southgate amepongeza ushindi dhidi ya Ukraine lakini amekiri kuwa mechi dhidi ya Denmark itakuwa ngumu zaidi kwa kikosi chake.

Mechi ya kwanza ya nusu fainali itachezwa katika uga wa Wembley, siku ya Jumanne tarehe 6 kati ya Uhispania na Italia. Kisha England itoane kijasho na Denmark Jumatano tarehe 7.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW