1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ENTEBBE : Serikali ya mpito Burundi yaongezewa muda

23 Aprili 2005

Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu barani Afrika hapo jana wameongeza muda wa mamlaka ya serikali ya mpito nchini Burundi kwa miezi minne zaidi hadi tarehe 26 mwezi wa Augusti tarehe ambayo Rais mpya anatazamiwa kuapishwa.

Baada ya mkutano huo Rais Museveni wa Uganda amewaambia waandishi wa habari kwamba kipindi cha serikali ya mpito kimeongezwa muda hadi Augusti 26 , chaguzi za taifa za serikali za mitaa na bunge zinatakiwa ziwe zimekamilikia ifikapo tarehe 19 mwezi wa Augusti na Rais kuapishwa hapo tarehe 26 mwezi wa Augusti.

Chini ya katiba Rais wa muda wa Burundi Domitien Ndayizeye ambaye ni Mhutu alikuwa lazima ajiuzulu mwishoni mwa kipindi cha mamlaka yake ambacho ilikuwa kimalizike hapo jana.

Mkutano huo pia umeidhinisha jitihada za Tanzania kulirudihsa kundi pekee la waasi wa Kihutu lililobakia nchini Burundi la FNL kwenye mazungumzo ya amani katika jaribio la kukomesha kabisa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya karibu miaka 12 nchini humo.

Marais waliohudhuria mkutano wa viongozi wa dharura mjini Entebbe Uganda ni pamoja na Marais wa Kenya,Zambia,Tanzania na Uganda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW