1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ENTERPRISE;Alabama : Kimbuga chauwa 18

2 Machi 2007

Kimbuga kimeuwa takriban watu 18 katika jimbo la Alabama nchini Marekani hapo jana wakiwemo wanafunzi 15 katika shule ya sekondari ambapo wanafunzi hao walikuwa wamenasa chini ya paa lililoanguka.

Watu wawili walikufa mahala pengine katika mji wa Enteprise na mmoja katika eneo la kijijini la Millers Ferry .

Msemaji wa shirika la kushughulikia Masuala ya Dharura ya Jimbo la Alabama Yasamie Richardson amesema idadi ya maafa inaweza kuongezeka wakati juhudi za uokozi zikiendelea wakati wa usiku.

Zaidi ya watu 50 wamelazwa hospitali kutokana na kimbunga hicho kikali kupiga jimbo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW