Enzi ya Edmund Stoiber yamalizika
29 Septemba 2007Matangazo
Stoiber pia anamaliza awamu ya miaka 14 kama waziri mkuu wa jimbo la Bavaria,baada ya kushinikizwa na wanachama wenzake kwa miezi kadhaa.
Uongozi wa chama cha CSU unagombewa na wanachama watatu:Waziri wa Uchumi wa Bavaria,Erwin Huber;Waziri wa Kilimo wa Ujerumani,Horst Seehofer na Gabriele Pauli ambae juma lililopita alihoji maadili ya chama hicho,kuhusu masuala ya familia.Bibi Pauli alishauri kuwa ndoa zidumu kipindi cha miaka saba.
Günther Beckstein ambae hivi sasa ni Waziri wa Ndani wa jimbo la Bavaria,anamrithi Stoiber kama waziri mkuu wa jimbo hilo.