Enzi za TP Mazembe kimataifa zinafifia
12 Mei 2025
Ligi kuu nchini DRC iliendelea mwishoni mwa wiki katika hatua ya mtoano ili kusaka bingwa wa ligi kuu na timu 4 zitakazo tinga kwenye michuano ya mabingwa na shirikisho barani Afrika.
Klabu ya TP Mazembe imepata kipigo Cha pili mfululizo suala ambalo linaiweka klabu hiyo katika njia panda ya kushiriki mashindano ya Afrika.
Hali ilikuwa nzuri kwa vijana wa Jimbo la Tanganyika kwa kuwafunga TP Mazembe kwenye uwanja wao mabao 2-1, suala ambalo limewapa wakati mgumu mabingwa watetezi Tp Mazembe ambao wamepoteza mechi 3 katika mechi 6 za hivi karibuni na 2 mfululizo kwenye uwanja wao.
Soma zaidi:Droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika yafanyika Cairo
Kocha wa timu ya Tanganyika, Saber Ben Jabria aliwamwagia sifa wachezaji wake.
"tumekuja hapa na tumecheza, tumecheza vyema, hatukustahili kupoteza kwa mara ya pili mbele yao, kwanza nawashukuru wachezaji wangu, kwakweli ni sababu yao na kupitia mbinu walizoonesha za hali ya juu, walifanya kazi yao vyema, walikuwa juu"
Mashabiki wa FC Tanganyika Jimboni hapa walionekana kufurahia matokeo hayo.
Wachambuzi wana hofu juu ya matokeo haya
Wachambuzi nchini wanahofia kupata wawakilishi tofauti kwenye mashindano ya Mabingwa na shirikisho barani Afrika
Ramazani kahambwe anahofia kuipoteza TP Mazembe kwenye anga za kimataifa.
''Kutokana na kiwango alichokionesha msimu huu TP Mazembe ni ngumu sana kwenda klabu bingwa kwasababu kuna timu zingine ambazo zimewekeza, kama Les Aigles du Congo, Maniema"
Eric kayumba "kwetu sisi kama watoto wa Tanganyika tumefurahi kuona timu ya nyumbani inamlaza bingwa mtetezi, tunaamini mwisho utakuwa mzuri"
Soma zaidi:Wydad Casablanca mabingwa CAF Super Cup
Kutokana na kiwango alichokionesha msimu huu TP Mazembe ni ngumu sana kwenda klabu bingwa kwasababu Kuna timu zingine ambazo zimewekeza, kama Les Aigles du Congo, Maniema"
Aruna Anzuruni ni mkaazi wa kisebwe mjini kalemie, upande wake ameiambia DWkuwa hatua ya timu ya Tanganyika kuifunga TP Mazembe ni suala kupongeza na kutupatia matumaini kwani ni msimu wa kwanza kushiriki ligi hii"
Matokeo mengine ni Yale ya Don Bosco 2-1 DCMP Sanga Balende 1-1 As Simba Kolwezi Maniema Union 2-0 Rangers Vita club 1-0 Anges Verts.
Maniema Union anashikilia nafasi ya kwanza, St Eloi Lupopo ya 4, TP Mazembe nafasi ya 5, FC Tanganyika nafasi ya 8.