1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan aapishwa tena kuwa rais wa Uturuki kwa miaka mitano

3 Juni 2023

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameapishwa kwa mara nyengine tena mjini Ankara, kuwa rais wa Uturuki kwa miaka mingine mitano, baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.

Türkei, Ankara | Recep Tayyip Erdogan, Amtseid & Einweihungszeremonie
Picha: Umit Bektas/REUTERS

Wakati wa kiapo chake Erdogan amesema atakubali maoni  ya wananchi na kuheshimu haki za binaadamu. Upande wa upinzani haukusimama wakati rais huyo wa Uturuki alipokuwa anakula kiapo cha kuchukua tena madaraka. 

Erdogan ashinda duru ya pili ya uchaguzi Uturuki

Erdogan, anayeingia kwenye muhula wa tatu madarakani, anatarajiwa kulitangaza baraza lake la mawaziri baada ya sherehe za uapisho. Katika uchaguzi wa wiki iliyopita uliomuweka madarakani, Rais huyo wa Uturuki aliungwa mkono kwa asilimia 52. 

Sherehe za uapisho zitafuatiwa na hafla itakayofanyika katika kasri la Rais na inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi kutoka mataifa 78, na mashirika ya kimataifa. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW