1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Erdogan ameashiria ataunga mkono kuikaribisha Finland NATO

30 Januari 2023

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameashiria ataunga mkono mchakato wa kuikaribisha Finland ndani ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO huku akizuia kutoa ridhaa ya kuipatia Sweden ndani ya jumuiya hiyo ya kijeshi.

 Recep Tayyip Erdogan
Picha: Emin Sansar/AA/picture alliance

Katika hotuba aliyoitoa kwa ajili ya vijana wa Uturuki, Erdogan amesema nchi yake inaweza kuridhia Finland kuwa mwanachama wa NATO lakini siyo Sweden, anayoituhumu kuyaunga mkono makundi yaliyopigwa marufuku nchini Uturuki.

Soma pia:Uturuki yachukuwa hatua dhidi ya uchomaji Quran barani Ulaya

Ingawa serikali ya Erdogan inayalaumu mataifa yote mawili kwa kuwasaidia wapiganaji wa Kikurdi nchini Uturuki, msimamo wake kuelekea Sweden umetiwamakali na kitendo cha wiki iliyopita ambapo mwanasiasa wa mrengo mkali nchini Sweden aliichoma moto Quran Tukufu  mbele ya ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm.

Kufuatia kitendo hicho Erdogan alisema Sweden haiwezi tena kuitegemea Uturuki kuisaidia kupata unachama wa NATO.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW