SiasaUturuki
Erdogan aonya Sweden kuhusu NATO baada ya kuchomwa Quran
24 Januari 2023Matangazo
Kauli za hasira zilizotolewa na Rais Erdogan zimezidi kuyafifisha matarajio ya Sweden na Finland kujiunga na muungano huo wa ulinzi wa mataifa ya magharibi, kabla ya uchaguzi wa rais na bunge nchini Uturuki wa mwezi Mei.
Erdogan amesema ikiwa Sweden inawapenda sana wanachama wa mashirika ya kigaidi na maadui wa Uislamu, basi ipeleke masuala ya usalama wake kwao.
Marekani imesema tukio hilo la kuchukiza la kuchomwa Quran lililofanywa na mfuasi wa itikadi kali za mrengo wa kulia huenda lililenga kuhujumu umoja ndani ya NATO.