1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan awataja wagombea wa chama katika uchaguzi wa Machi

Josephat Charo
7 Januari 2024

Rais Erdogan anamuunga mkono waziri wa zamani wa mazingira Murat Kurum kwa matumaini ya kuutwaa mji wa Istanbul kutoka kwa upinzani.

Türkei Präsident Recep Tayyip Erdogan und Murat Kurum in Istanbul
Rais Erdogan, kulia, na Murat Kurum, kushoto, mjini Istanbul 07.01.2024Picha: Murad Sezer/REUTERS

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewataja wagombea kadhaa wa chama chake watakaowania nafasi katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Machi. Chama tawala kitajaribu kujiimarisha na kuitwaa miji iliyochukuliwa na chama cha upinzani cha Republican People, CHP, miaka mitano iliyopita, ukiwemo mji mkubwa kabisa wa Uturuki, Istanbul, na mji mkuu, Ankara.

Erdogan amesema mbunge na waziri wa zamani wa mazingira na ukuaji wa miji, Murat Kurum, atapambana na Ekrem Imamoglu, meya wa upinzani wa mji wa Istanbul, ambaye ametambuliwa kitaifa. Wengi walitarajia Imamoglu kushindana na Erdogan katika uchaguzi wa rais mwaka uliopita. Erdogan ameuambia mkutano mkuu wa chama tawala, Justice and Development -  AKP - mjini Istanbul kwamba mji huo utafanikiwa kutimiza azma yake na hauwezi kupoteza kwa miaka mingine mitano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW