1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan: Ethiopia na Somalia wameafikiana kumaliza mzozo

12 Desemba 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amesema viongozi wa Somalia na Ethiopia wamefikia makubaliano ya kumaliza mzozo uliodumu kwa takribani mwaka mmoja.

Uturuki|Ethiopia|Somalia| Mazungumzo
Moja ya duru za mazungumzo ya kumaliza uhasama kati ya Ethiopia na Somalia yaliyokuwa yakiratibiwa na Uturuki.Picha: Arda Kucukkaya/Anadolu/picture alliance

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo yaliyofanyika jana Jumatano, kwa saa kadhaa mjini Ankara.

Akiyasifu makubaliano hayo ya kihistoria katika mkutano wa pamoja na waandishi habari, Erdogan amesema ana matumaini kwamba mpango huo utakuwa hatua ya kwanza kuelekea mwanzo mpya unaozingatia amani na ushirikiano kati ya Somalia na Ethiopia.

''Pamoja na michango ya nchi zote mbili, tumeandaa tamko la pamoja ambalo tumekubaliana leo. Tamko hili la pamoja linarekodi kanuni ambazo nchi hizi mbili rafiki, zilizo muhimu sana kwetu katika kuziangazia siku zijazo, na sio yaliyopita. Na haya yatafanywa kuanzia sasa.'' amesema kiongozi huyo.

Erdogan amewashukuru Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kwa kufikia makubaliano hayo ya kihistoria. Amesema Ethiopia na Somalia zina nia ya kushirikiana pamoja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW