1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan kukutana na Putin mjini Moscow

4 Septemba 2023

Ziara ya Erdogan ni muhimu katika kujaribu kuufufua mkataba wa kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki.

NATO-Gipfel in Vilnius Erdogan
Picha: LUDOVIC MARIN/AFP

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anakutana leo na rais wa Urusi Vladimir Putin kujadili mkataba wa kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi. Mshauri mkuu wa sera ya kigeni wa Erdogan, Akif Cagatay Kilic amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha A Haber kwamba wanashuhudia uungwaji mkono mkubwa kote ulimwenguni huku Uturuki ikipania kuirejesha Urusi kwenye mkataba huo uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Ututuki  iliyojiondoa mnamo mwezi Julai mwaka huu.

Hapo jana maafisa wa Ukraine walisema ndege za Urusi zisizo rubani ziliharibu miundombinu katika bandari ya mto Danube ambayo ni muhimu kwa usafirishaji nje wa nafaka ya Ukraine, ambapo watu wawili walijeruhiwa kusini mwa eneo la Odesa. Mto huo umekuwa njia kuu ya usafirishaji nje wa nafaka ya Ukraine tangu Urusi ilipojiondoa kutoka kwa mkataba huo.

(Reuters)