Erdogan kumshawishi Putin kufufua mkataba wa nafaka Ukraine
4 Septemba 2023Urusi inadai nchi za Magharibi zinapaswa kuiondolea vikwazo vinavyoharibu biashara yake ya kilimo.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikaa kwa muda wa saa tatu kwenye mazungumzo na kiongozi huyo wa Urusi akijaribu kumshawishi kufufua makubaliano hayo ya usafirishaji nafaka kutoka Ukraine kupitia bandari tatu za eneo la bahari nyeusi,licha ya vita.
Soma pia:Putin kukutana na Erdogan mjini Sochi
Mkutano huo uliofanyika katika mji wa Sochi, umefanyika katika wakati ambapo hivi karibuni Ukraine ilianzisha mashambulizi ya kujibu mapambano dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Tangu rais Putin alipojiondowa katika mkataba huo wa usafirishaji nafaka ,Erdogan amekuwa akiaahidi kufanya mipango ya kusaidia kuyafufua ili kuepusha mgogoro wa chakula katika baadhi ya nchi za Kiafrika,Mashariki ya Kati na Asia.