Erdogan: PKK kusalimisha silaha ni ukurasa mpya kwa Uturuki
12 Julai 2025
Matangazo
Wanamgambo thelathini wa PKK, jana walichoma moto silaha zao kwenye lango la pango moja kaskazini mwa Iraq, kuashiria hatua muhimu kuelekea kumaliza uasi uliodumu kwa miongo kadhaa nchini Uturuki.
Akihuwatubia wanachama wa chama chake cha AK mjini Ankara, Erdogan, amesema kufikia jana, kero la ugaidi lilianza mchakato wa kukamilika na kwamba leo, milango ya Uturuki iliyo imara imefunguliwa.
PKK yatangaza kuweka chini silaha
Rais huyo ameongeza kuwa hatua za hivi karibuni, zimeliunganisha taifa hilo na kwamba sasa bunge litatekeleza jukumu muhimu katika kuunda mfumo wa kisheria wa kukamilisha mchakato wa usalimishaji silaha.