Eritrea yakatiza uanachama wake wa IGAD
13 Desemba 2025
Katika taarifa yake, wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imesema Eritrea imejiondoa kutoka kwenye jumuiya ya IGAD kwa sababu imeona kuwa jumuiya hiyo imepoteza jukumu na mamlaka yake ya kisheria, kutokuwa na faida yoyote ya kimkakati kwa wanachama wake na pia kushindwa kuchangia kikamilifu kwa utulivu wa eneo hilo.
Eritrea ilijiondoa IGAD mwaka 2003 na kujiunga tena miaka miwili iliyopita, lakini imesema kwamba jumuiya hiyo imeshindwa kuleta utulivu wa kikanda.
Kwa upande wake, IGAD imejibu kwa kusema Eritrea haijashiriki katika shughuli za kikanda tangu ilipojiunga tena na jumuiya hiyo.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi kuhusu kuzuka upya kwa mvutano kati ya Eritrea na nchi jirani ya Ethiopia, ambazo zilitia saini makubaliano ya amani miaka 25 iliyopita.