Esther Zawadi Panga, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
23 Mei 2013Matangazo
Umoja wa Afrika ni jumuia kongwe. Kwetu sisi Waafrika, hauna maana yoyote. Unahitaji kuangalia nchi kama Mali tu, utaona badala ya Umoja wa Afrika, Ufaransa ndio iliyoingilia kati. Nchini mwetu, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa zaidi ya miaka 10 tunaishi katika vita. Umoja wa Afrika ungebidi ulete wanajeshi wake huku na sio Umoja wa Mataifa. Ninataraji Umoja wa Afrika utafanyiwa marekebisho. Kwa sababu hauchangii kuyapatia ufumbuzi matatizo ya bara la Afrika.