1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Estonia: Umoja wa Mataifa kujadili uchokozi wa Urusi

22 Septemba 2025

Estonia imesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya kikao cha dharura kujadili ukiukaji wa usalama wa anga yake uliofanywa na ndege za kivita za Urusi.

Estonia Ghuba ya Finland 20255 | Ndege ya kivita ya Urusi chapa MiG-31
Ndege ya kivita ya Urusi MiG-31 ilikiuka usalama wa anga ya EstoniaPicha: Forsvarsmakten/AFP

Kitendo cha Urusi kukiuka usalama wa anga ya Estonia kilikosolewa vikali na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Siku ya Ijumaa, vikosi vya Jumuiya ya Kujihami ya NATO, vilizizuia ndege tatu za kivita za Urusi chapa MiG-31, baada ya kuingia katika anga ya Estonia kwenye Ghuba ya Finland.

Hatua hiyo ilisababisha malalamiko ya uchokozi mpya unaoleta hatari katika nchi za NATO na Umoja wa Ulaya, madai yaliyokanushwa na Urusi.

Wakati huo huo, kikosi cha anga cha Ujerumani kimesema kimepeleka ndege mbili za kivita kuifatilia ndege moja ya kijeshi ya Urusi chapa IL-20m iliyoingia katika anga ya Bahari ya Baltic Jumapili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW