1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Estonia yaongeza vikwazo dhidi ya viongozi wa Georgia

16 Desemba 2024

Estonia imetangaza vikwazo ziada jana Jumapili vinavyowalenga viongozi wa kisiasa nchini Georgia.

Maandamano ya Georgia
Maandamano ya Georgia.Picha: Alexander Patrin/TASS/dpa/picture alliance

Nchi hiyo imesema hatua hiyo ni jibu kwa ukandamizaji uliofanywa na watawala wa Georgia dhidi ya maandamano ya kuunga mkono mahusiano ya karibu na Umoja wa Ulaya.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Estonia imesema vikwazo hivyo vya nyongeza vinawahusu maafisa 14 wanaobebeshwa dhima ya kuwakabili waandamanaji kwa mabavu. Miongoni mwao ni Waziri Mkuu wa Georgia, Irakli Kobakhidze, ambaye yeye na wenzake 13 watazuiwa kuingia Estonia.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Estonia, Margus Tsahkna, amesema nguvu ambazo mamlaka za Georgia zinatumia "kuwakabili waandamanaji, waandishi habari na viongozi wa upinzani hazikubaliki."

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Estonia pia ametoa rai kwa nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Ulaya kuchukua hatua nzito dhidi ya wote wanaotumia nguvu kupita kiasi kuzima maandamano ya Georgia.

Maandamano yalizusha nchini Georgia mnamo mwezi Oktoba baada ya Waziri Mkuu Kobakhidze kutangaza uamuzi wa kuchelewesha mazungumzo ya nchi yake kujiunga na Umoja wa Ulaya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW