1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaeSwatini

Eswatini yafanya uchaguzi wa Bunge

29 Septemba 2023

Eswatini ambayo ni nchi pekee iliyobakia barani Afrika yenye utawala kamili wa kifalme, imefanya hii leo uchaguzi wa bunge huku vyama vya kisiasa vikiwa vimezuiwa kushiriki.

Raia wa Eswatini wakipiga kura
Raia wa Eswatini wakipiga kuraPicha: Marco Longari/AFP via Getty Images

Raia wa Eswatini watawachagua wabunge 59 wa baraza la Bunge, ambalo lina jukumu pekee la kumshauri Mfalme.

Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa siku chache zijazo, na upinzani nchini Eswatini ambayo awali ilifahamika kama Swaziland, umetoa wito wa kususia upigaji kura.

Vyama vya kisiasa vimepigwa marufuku katika nchi hiyo na wabunge hawawezi kuhusishwa na makundi ya kisiasa.

Zaidi ya watu 500,000 wamejiandikisha kupiga kura katika taifa hilo maskini la kusini mwa Afrika, ambako Mfalme Mswati III aliyeingia madarakani tangu mwaka 1986, amekuwa na mamlaka kamili.

Licha ya maandamano ya mwaka 2021 ya kudai demokrasia, uwezekano bado ni mdogo wa kubadilisha hali ya kisiasa katika ufalme huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW