1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaeSwatini

Eswatini yajiandaa kufanya uchaguzi wa wabunge

26 Septemba 2023

Nchi pekee iliyobakia barani Afrika yenye utawala kamili wa kifalme, Eswatini, Ijumaa wiki hii itafanya uchaguzi wa bunge huku vyama vya kisiasa vikiwa vimezuiwa kushiriki uchaguzi huo.

Pichani ni Mfalme wa Eswatini,  Mswasti III
Pichani ni Mfalme wa Eswatini, Mswasti III Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Nchi pekee iliyobakia  barani Afrika yenye utawala kamili wa kifalme, Eswatini, Ijumaa wiki hii itafanya uchaguzi wa bunge huku vyama vya kisiasa vikiwa vimezuiwa kushiriki uchaguzi huo.

Katiba ya nchi hiyo inasisitiza juu ya kile kinachoitwa ''kigezo cha mtu binafsi'' kama msingi wa kuchaguwa wabunge, ambao hawafungamanishwi na kundi lolote la kisiasa.

Soma pia:Umoja wa Mataifa yaitisha uchunguzi kufuatia mauaji ya Eswatini

Kadhalika watu wanaokubalika kwa Mfalme Mswati wa Tatu mwenye mamlaka yote ya uongozi nao wako katika nafasi nzuri. 

Takribani wapiga kura 585,000 waliojiandikisha watashiriki kuchagua wabunge 59. Bunge la Eswatini lina jukumu moja tu, ambalo ni kutowa ushauri kwa ufalme.

Nafasi ya vyama vya kisiasa haijafafanuliwa wazi nchini humo na ndio sababu haviruhusiwi kushiriki moja kwa moja katika uchaguzi. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW